Mark 12:38-40

Yesu Awatahadharisha Watu Kuhusu Walimu Wa Sheria

(Mathayo 23:1-36; Luka 20:45-47)

38 aAlipokuwa akifundisha, Yesu alisema, “Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni. 39 bPia wao hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kupewa nafasi za heshima katika karamu. 40 cWao hula nyumba za wajane, na ili waonekane kuwa wema wanasali sala ndefu. Watu kama hawa watapata hukumu iliyo kuu sana.”

Copyright information for SwhNEN